Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland ya nchini Norway kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wagonjwa wa akili, Kidongo Chekundu ambayo itakuwa ya kisasa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland ya nchini Norway ukiongozwa na Trond Mohn aliyefuatana na rafiki zake pamoja na familia yake wakiwa pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya.
Rais Dk. Shein alisema kuwa hiyo ni habari njema na ya kujivunia inayotokana na uhusiano, ushirikiano na urafiki wa muda mrefu unaoendelezwa kati ya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland ya nchini Norway na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Aliongeza kuwa Hospitali ya wagonjwa wa akili iliyopo Kidongo Chekundu ni hospitali kongwe katika hospitali kadhaa hapa nchini ambayo ina historia kubwa inayotokana na utoaji huduma zake kwa wakati huo ilipojengwa na wakoloni wa Kiengereza mnamo miaka ya 50 ambapo ilipewa jina na jamii kwa kuitwa “Jela ya Wendawazimu”.
Hivyo, hatua za kuijenga upya Hospitali hiyo na kuwa ya kisasa na ya pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itakuwa ni faraja kubwa kwa Wazanzibar kwa kuiimarisha sambamba na kutoa huduma za kisasa za wagonjwa wa akili na kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi.
Friday, November 22, 2019
Home
/
Top News
/
Rais Dk. Shein aupongeza uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland ya nchini Norway
Rais Dk. Shein aupongeza uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland ya nchini Norway
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment