Adbox

Friday, November 22, 2019

Naibu Waziri Kanyasu aanza kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa CCM

Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameanza kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Chama cha Mapinduzi( CCM) kwa wananchi kwa ajili ya  uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika  mwishoni mwa wiki hii.


Akizungumza na Wananchi wa eneo la  Mpomvu katika Kata ya Mtakuja mkoani Geita, Kanyasu ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka minne.

Katika mkutano huo, Kanyasu amewatambulisha Wenyeviti wateule wa mitaa saba kwa wananchi na kuwataka watoe ushirikiano ili kuleta maendeleo.

Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana katika nyanja ya Elimu, Afya, Barabara, mikopo pamoja na Umeme.

Mbali ya kuelezea mafanikio hayo yaliyopatikana katika utekezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015-2020) katika jimbo hilo, Kanyasu ametaka wananchi kutoa ushirikiano kwa  Wenyeviti wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo ili kuharakisha miradi ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Adbox