Mahakama nchini Argentina imewahukumu makasisi wawili wa Kanisa Katoliki la Roma kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela kila mmoja v kwa kuwanyanyasa kingono watoto viziwi katika shule ya kanisa.
Horacio Corbacho na Nicola Corradi, pamoja na muhudumu wa bustani, walipatikana na hatia ya kuwabaka na unyanyasaji wa kingono katika shule hiyo ya kikatoliki iliyopo katika jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.
Waathiriwa kadhaa walikuwa mahakamani kushuhudia kutolewa kwa hukumu Jumatatu.
Kesi hiyo imeishitua Argentina, nchi ambayo anatoka Papa Francis, huku wengi wakilishutumu kanisa kwa kuzorota kuchukua hatua.
Kanisa hilo limekabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono wa watoto katika maeneo mbalimbali duniani kipindi cha miongo michache iliyopita.
Tuesday, November 26, 2019
Makasisi wahukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kuwanyanyasa watoto kingono
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment