Rais John Magufuli ametoa siku 60 kuanzia leo Taasisi na Mashirika ya Umma 187 yaliyoshindwa kukabidhi gawio na michango yao kuhakikisha wanakabidhi gawio hilo vinginevyo viongozi wake wajiondoe wenyewe.
Ametoa agizo hilo leo Ikulu jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango kutoka katika Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma ambapo amepokea shilingi Trilioni 1.05 kutoka kwa taasisi na mashirika 79 kati ya 266.
Amesema kuwa Serikali imewekeza shilingi trilioni 59.6 kwa taasisi na mashirika 266 lakini kutokana na utendaji mbovu,ufuatiliaji dhaifu na vitendo vya wizi,rushwa na ubadhirifu kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa mapato yaliyokusanywa kupitia uwekezaji huo yalikuwa madogo.
“Hatuwezi kuendelea kuwa na Mashirika au Taasisi za namna hii, pamoja na wenyeviti wa Bodi, tunazungumza kila mara hawataki kuelewa, licha ya Serikali kuweka fedha kiasi cha shilingi trilioni 59.6 ambazo ni fedha za watanzania kama mtaji katika Mashirika hayo, Waziri Mpango natoa siku 60 kuanzia leo ili Mashirika haya 187 yaweze kukabidhi kwako gawio” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha awaandikie barua wote ambao hawapo kwenye orodha hii, baada ya siku 60 ambaye hataleta gawio lolote ajihesabu hayupo, kila siku wanasema wanapata hasara, kila siku ni hasara tu, nchi za Scandinavia zinaendesha nchi zao kwa sababu ya gawio, wana watu waaminifu kama nyinyi mlioleta gawio hapa leo.
Sunday, November 24, 2019
Hatuwezi kuendelea kuwa na Mashirika au Taasisi za namna hii - Rais Magufuli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment