Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na nyingine kutokana na matumizi ya takwimu zenye viwango na ubora unaotakiwa,” - Mchumi Mwandamizi kutoka Benki ya Dunia, Nadia Belghith.
“Takwimu zinawawezesha wakulima kujua wapi yalipo masoko ya mazao yao hivyo kuchochea maendeleo yao na nchi kwa haraka zaidi,” alisisitiza Belghith .
Akifafanua amesema kuwa takwimu ni msingi na kichocheo cha maendeleo katika taifa lolote kama ilivyo kwa Tanzania ambayo katika Afrika ni ya pili kwa kuzalisha takwimu bora.
Ujumbe wa Benki ya Dunia na Ofisi ya NBS wamekutana Jijini Dodoma kwa wiki moja katika mkutano wa mashauriano wa kuimarisha ushirikiano wao.
Katika mkutano huo moja ya masuala yaliyozungumziwa ni kufanikisha utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Pili wa Taifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu (TSMP II) unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2019/ 2020.
Saturday, November 2, 2019
Benki ya Dunia yapongeza ubora wa Takwimu zinazozalishwa Tanzania
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment