Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amemuomba Rais John Magufuli kuwarejeshea fungu lao la fedha lililokuwa limetengwa ndani ya shilingi bilioni nne ambazo alizizuia kutoka HAZINA baada ya kugundua kuwepo kwa mchezo mchafu.
Bashe amesema, adhabu hiyo imewaathiri wao ambao hawakuhusika na mchezo huo huku tayari walikiwa wameshaanza mkakati wa kujenga mradi wa ujenzi wa kituo cha maegesho na kituo cha 'stop over' mjini Nzega.
Hata hivyo akijibu ombi hilo Rais Magufuli amesema, fedha hizo zilishapelekwa kwenye miradi mingine hivyo wasubiri mgao mwingine huku akikiri kuwa hakuwa na mpango wa kupita eneo hilo.
"Lakini nikiri nikuwa nisipite hii njia, ninahisi huyu Bashe amefanya ujanja na wanaotanguliza msafara..ameukwepesha nikaona naingizwa humu ndani. Sasa suala la maji umeshaanza....hili swala la stendi kwakweli niseme wazi, zile fedha zimeshapangiwa matumizi mengine" Rais Magufuli.
Wednesday, November 27, 2019
Bashe amuomba Rais Magufuli kuwarejeshea fedha alizowanyang'anya
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment