Adbox

Tuesday, October 29, 2019

Zlatan Ibrahimovic kurudi kucheza soka Hispania

Baada timu yake ya LA Galaxy kushindwa kufuzu fainali ya ukanda wa Magharibi katika MLS kwa kutolewa na Los Angeles FC, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic leo ameibua maswali mengi kuwa huenda anarejea LaLiga baada ya kuweka Video katika ukurasa wake wa Instagram akisema kuwa anarudi nchini Hispania.

Zlatan,38, ambaye mkataba wake na LA Galaxy unaisha mwezi Disemba mwaka huu,aliwahi kucheza LaLiga kati ya mwaka 2009 na 2011 akiwa na FC Barcelona.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Msweden huyo anarejea Serie A, huku klabu za Napoli, Bologna na Inter Milan zikuhusishwa kuwa ndio zinaisaka saini yake.

No comments:

Post a Comment

Adbox