Adbox

Thursday, October 17, 2019

Waziri Biteko atoa ahadi kwa kila mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza kidato cha Nne

Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini alihudhuria Mahafali ya 15 ya Shule ya Sekondari Busangi iliyopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya Kahama mkoani Shinyanga.


Akizungmza kwenye Mahafali hayo, Biteko alitoa ahadi ya mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo huku akiungwa mkono na viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala aliyeahidi kupeleka
Tsh. 25,000,000 (milioni 25) kwa ajili ya ujenzi huo.


Aidha Biteko aliahidi kutoa Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa
daraja la kwanza katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule hiyo ya Sekondari Busangi.

No comments:

Post a Comment

Adbox