Adbox

Monday, October 21, 2019

Waziri aitaka kampuni ya Advent Constructio limited kukamilisha ujenzi wa Mahakama kuu

Na Thabit Madai,Zanzibar.

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar,  Khamis Juma Maalim ameitaka kampuni ya Advent Construction Limited kutoka jijini  Dar es Salaam  kukamilisha kwa muda waliokubaliana Ujenzi wa Jengo la Mahakama kuu  iliyopo Tunguu Mkoa wa Kusini.

Amesema Ujenzi huo utachuuwa kipindi cha mwaka Mmoja ambapo Jengo hilo linatarajiwa kumalizikwa ifikapo mwaka 2020.

 Hayo aliyaeleza huko Mahakama Kuu Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya ghafla ya kutiliana saini na Kampuni ya Advent Construction ambayo inayotarajia kujenga Mahakama mpya Tunguu Mkoa wa Kusini  Unguja.


 Alisema kitendo cha kusaini mkataba huo ni muhimu sana  ikiwa  ni Utekelezaji wa  Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo  kusimamia na kuimarisha haki  ili wananchi wapate haki za kusimamia kesi zao.

Aliwataka  kujenga  jengo lenye ubora na kukamilisha  kwa muda uliopangwa ili wawe na jengo la kisasa na waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi  na kupata Mahakama iliyo nzuri Zanzibar ambapo inatarajiwa kumalizika hapo mwakani kabla ya Dkt Shein kumaliza uongozi wake ikiwa ni miongoni mwa  ahadi zake.

Pia alisema sheria ya msaada ishatungwa kwa lengo la kuandaa mazingira yaliyo mazuri kwa wananchi kupata haki zao kwa urahisi.

Hivyo aliwaomba wakandarasi hao kujenga jengo lenye ubora  na kiwango madhubuti ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kutarajia likimaliza litasaidia Serikali katika utendaji wake.

“Tunaomba jengo hili lijengwe kwa kiwango kilicho bora ili kuweza kudumu kwa muda mrefu na kuepuka kujenga jengo bila ya kiwango” alisema Waziri huyo.


Nae Jaji Mkuu Omar Othman Makungu aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanajenga Mahkama iliyo ya kupendeza ili na sie tuwe na Mahakama iliyo nzuri yenye sifa kwa Zanzibar na kufanya wafanyakazi kila kitendo kinapata sehemu ya kufanyia kazi kwa nafasi.

Alisema wanaishukuru  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujiandaa kutujengea jengo la Mahakama mpya kwa lengo la kutuimarishia miundo mizuri ya utendaji wa kazi kwa kila sekta.

“Tunashukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza  kutaka kutujengea   jengo hili kwani  jengo hili  sasa lishakuwa dogo halikidhi haja kwa wafanyakazi hivyo likimalizika huko tutaweza kufanya kazi zetu katika mazingira mazuri”, alisema Jaji huyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox