Adbox

Wednesday, October 30, 2019

Wazazi, walezi wanaowatanguliza watoto kutenda uhalifu kushugulikiwa

Na.Timothy Itembe Mara

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Saimon Sirro amekemea baadhi ya Wazazi na walezi wanaotanguliza Watoto wao katika kutenda uhalifu ambapo amesema kuwa wakibainika watashugulikiwa kisheria.

Sirro alisema  hayo leo katika mkutano wa hadhara alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mji wa Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara juu ya masuala ya ulinzi na usalama wa Raia na mali zao.

“Nimepata taarifa kuwa kuna baadhi ya wazazi na walenzi ambao wanawatanguliza watoto wao katika kutenda uhalifu hususani kuingia mgodini kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu watoto hao wakibainika,wazazi au walezi wao wote kwa pamoja watachukulia hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kupelekwa mahakamani kushitakiwa“alisema Sirro.

Mkuu huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka watoto waliochini ya umri wa miaka 18 wote ambao sio wakazi wa Nyamongo (WALOWEZI) kurudi makwao walikotoka vinginevyo jeshi hilo litawakamata na kuwashugulikia.

Kwa upande wake, Kamanda Mkoa wa Kipolisi,Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe alisema kuwa atatekelezxa agizo lililotolewa na mkuu wake wa kazi ili sheria kufuata mkondo wake.

Mwaibambe aliongeza kuwa mkoa kipolisi Tarime na Rorya nisalama lakini kuna changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wananchi kuvamia mgodi wa madini ya dhahabu uliopo Nyamopngo kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu suala ambalo nikinyume cha sheria.

Kamanda huyo aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao bado wanatenda ukatili wa kijinsia wakiwapiga wanawake zao na kuwakata mapanga masikio huku matukio mengine ni pamoja na  wakibakia watoto wakike na wengine kuwapachika mimba watoto wa shule.

Kwa mwaka 2018 matukio yaliyoripotiwa ya ukatili wa wanawake kupigwa na kukatwa na wanaume zao pamoja na watoto kubakwa ni zaidi ya matukio 30 na kwa mwaka huu ni tukio moja aliongeza kusema Mwaibambe.

Naye Diwani Viti Maalumu Kata ya Matongo kupitia Chama cha Demokorasia na maendeleo(CHADEMA), Filomenha Tontora alisemas kuwa kuna matukio mengi ya ukatili wa kijinsia Nyamongo ikiwemo wanawake kupigwa na kuteswa huku  kudhalalishwa hususani wale ambao wanauza vinywaji katika baa.

Diwani huyo aliongeza kuwa jamii ya watu wa Nyamongo wanayodharau ya kudharau viongozi mbalimbali pale ambapo wankuwa na ujumbe wa kuwatakia mambo ya kimaendeleo

No comments:

Post a Comment

Adbox