Adbox

Saturday, October 26, 2019

Wananchi watakiwa kutumia vyema wiki ya sheria

Na. Rahel Nyabali, Tabora

Kufuatiwa wiki ya sheria nchini wananchi mkoani tabora wametakiwa  kutumia wiki hiyo vyema ili kuweza kupata msaada wa kisheria hasa wasio na uwezo  kujua  matatizo  yanayowakabili  yanayohitaji  msaada  wa  kisheria  kwakuwa  wengi  wao  wamekuwa  wakijikuta  wanapoteza  haki  zao  kutokana  na kutojua  sheria  hasa  wanapokuwa  wakikabiliwa  na  mashauri  mbalimbali  mahakamani.


Hayo yameelezwa katika mdahalo ulio hudhuliwa na wadau mbalimbali mkoani humo    wakati  ambapo  Chama  cha  Wanasheria  TLS kanda  ya  Tabora  kikiwa  katika  wiki  ya  msaada  wa kisheria  kimeadhimidhimisha  wiki  hiyo  kwa  kufanya  mijadala  juu  ya  umuhimu  wa  Sheria  ya  msaada  wa  kisheria  ambapo  kimsingi  wananchi  hasa  wanyonge  wanapaswa  kufaidika  nayo.

Charles  ayo ni mmoja wa Wakili wa Kujitegemea mkoani Tabora amesema kufuati wiki  hii ya sheria ambapo wameweza  kukutana baadhi ya wananchi na wadau wa masuala ya kisheria katika  mjadala  unaohusu Sheria ya msaada wa kisheria  na  umuhimu wake  hasa  kwa  wananchi  wenye  mahitaji na wasio na uwezo kutaweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kupata uelewa kwa wananchi na kujua haki zao.

Mkazi  wa  Tabora Sophia  martin  ni moja ya mwananchi aliye pata wasaa wa kuchangia kwenye mdahalo huo amesema watu wengi hasa wa kijijini kwa kiasi  kikubwa hawana elimu juu ya huduma ya sheria hivyo amewaomba wanasheria kuwafikia watu hao ili kupata haki zao.

 Hata hivyo katika  kuadhimisha wiki ya msaada wa kisheria Chama cha Wanasheria TLS Kanda  ya Tabora wmeweza  kufika katika magereza ya Urambo,Nzega  na Gereza  kuu  la  Uyui  ili  kubaini mahitaji ya msaada wa kisheria kwa watu waliopo Magerezani. 

No comments:

Post a Comment

Adbox