Adbox

Friday, October 25, 2019

Waitara awapongeza ALAT

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mwita Waitara, amesema serikali inatambua mchango mkubwa inayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ALAT hapa nchi katika Mamlaka za Mitaa.


Waitara ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa Mamlaka za Serikali za Mitaa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki,EALGA  kutathmini na kubadilishana mawazo namna ya kuimarisha Mamlaka  miongoni mwa Mamlaka hizo.

Amesema Kama serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mamlaka hizo na Serikali ya Tanzania inafanya kazi kwa karibu na mamlaka ya serikali za mitaa katika kuhakikisha Sera ya Ugatuaji wa Madaraka itatekelezwa kwa asilimia 100.

"Serikali inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Mamlaka,  imekuwa ikishirikiana na ALAT katika kuboresha masuala ya utawala bora, utoaji wa huduma, kuondoa umasikini ili kuhakikisha mpango wa maendeleo enedelevu unafikiwa" amesema Waitara.

Waitara amesema serikali ipo tayari  kuchukua nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Nchi za Afrika Mashariki pindi nchi ya Rwanda uitakapomaliza muda wao ifikapo Mei 2020.

Aidha Waitara amewataka wanachama wa EALGA kutumia mkutano huo kubadilishana uzoefu katika maeneo ya utetezi, ushawishi, utoaji wa huduma, usambazaji wa habari zinazohusu Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Nchi za Afrika Mashariki (EALGA) Gulam Mukadamu, wakati wa kikao hicho amewaomba wakuu wa nchi wanachama ya Jumuia ya Afrika Mashariki kuendelea kuhakikisha kunakuwa na ugatuaji wa madaraka na kusaidia huduma za mitaa.

Amesema ni vyema EALGA ikaendelea kuwahimiza wakuu wa nchi wanachama wa utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuongeza juhudi za ugatuaji madaraka na kuongeza msaada wa kuboresha huduma za serikali za mitaa ili kuwa na taasisi imara ya serikali za mitaa.

Aidha ameishukuru  Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutekeleza Sera ya ukaguati madaraka katika ngazi ya serikali za mitaa.

Pia amewahimiza mawaziri wanaohusika na serikali za mitaa na jumuia za serikali za mitaa yakiwemo mabaraza ya madiwani kwa nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia kuwekeza katika uimara wa EALGF na EALGA.

No comments:

Post a Comment

Adbox