Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Tanga (TAKUKURU) imetoa onyo kwa wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ambao watajitoa dakika za mwisho.
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba alitangaza kiama kwa wagombea hao wakati akitoa taarifa ya taasisi hiyo ya mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu kwa Mkoa wa Tanga alipozungumza na waandishi wa habari.
Mariba alielezea mikakati ya taasisi hiyo kuelekea uchaguzi zijazo itafanyia kazi mambo ambayo chaguzi za awali zilizopita yalikuwa yakifanywa kiholela na kinyume cha sheria.
Kwenye chaguzi za serikali za mitaa Novemba 24 mwaka huu na mwaka 2020 hatutakuwa na mgombea atakayejitoa dakika za mwisho na atakayefanya hivyo hatua kali zitachukuliwa kwake.
Friday, October 18, 2019
Wagombea serikali za mitaa waonywa kuhusu rushwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment