Adbox

Saturday, October 19, 2019

Waendesha pikipiki watajwa kuchangia mimba mashuleni

Na Timothy Itembe Mara.

Mkuu wa shule ya sekondari Mogabiri halmashauri ya Mji wa Tarime,Magudira  Mugeta amesema kuwa waendesha Pikipiki maafuru kama (Bodaboda) wanachangia kuwapa mimba watoto wa kike mashuleni huku wakikatisha  masomo yao.

Mugeta alisema hayo jana mbele ya mgeni rasimi Burure Burito ambaye alialikwa  kuwa mgeni rasimi katika maafali ya 22 ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mogabiri wanaotarajia kufanya mitihani yao ya kuhitimu kidato cha Nnee  Novemba 04,2019.


“Ndani ya shule yangu kuna kesi mbili za wanafunzi  wa kike  wa kidato cha kwanza kudaiwa  kuwa wamepachikwa  mimba na  waendesha Pikipiki ambapo kesi hizo tiyari tumezipeleka sehemu husika na zinashugulikiwa naomba Serikali kuingilia kati swala hilo  ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake licha ya kuwa watu wa hapa Mogabiri wanatabia ya kulindana pindi kesi kama hizo zinapotokea”alisema Mugeta.

Mugeta aliendelea kufafanua kuwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nnee mwaka huu katika shule ya sekondari Mogabiri ni watoto 191 huku wasichana wakiwa 187 na wavulana ni 111.

Mkuu huyo alimaliza kusema kuwa shule yake inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa Sayansi hususani walimu wamasomo ya Fizikia na hisabati na kuwa shule yake masomo
yanayofundishwa ni pamoja na
Biolojia,Kiswahili,Kiingereza,Fizikia,Chemia,Uraia,Hisabati,Compyuta,fasihi ya kingereza na historia.

Kwa upande wake mgeni rasimi wa maafali hayo Burito Burure ambaye ni mkurugenzi wa Taasisi ya Tayana iliyopo Der-esalaamu aliomba jamii kwa kushirikiana na serikali ili kuendelea kumlida mototo wa kike na pindi inapo bainika kupewa mimba watuhumiwa washugulikiwe kisheria bila kuoneana aibu za koo na kulimaliza kienyeji.

Burito aliendelea kuitaka jamii ya kabila la wakurya kuacha tabia ya kulindana pande mbili kwa maana ya upande wa msichana na upande wa mvulana  pindi tatizo la kupewa mimba kwa  mototo wa kike linapokuwa limetokea  na  badala yake swala hilo limalizwe kisheria badala ya kinyumbani.

Naye Afisa mtendaji kata ya Kenyamanyori,Rozimeri Chacha alikemea utoro mashuleni pamoja na mimba mashuleni swala ambalo alisema kuwa  swala hilo ni kikwazo  cha masomo kwa mototo wa kike na linapotokea  ni kikwazo cha kukwamisha  watoto wa kike kutimiza ndoto zao za kimasomo na kimaisha .

No comments:

Post a Comment

Adbox