Na Thabit Madai,Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Amina Salum Ali ameitaka Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chamber of commerce) kuitumia fursa walioipata ili kuingia katika ushindani wa kibiashara Kanda ya Afrika Mashariki.
Hayo aliyasema huko katika ukumbi wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Migombani wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo katika kujipanga namna ya kuikabili fursa hiyo.
Alisema Serikali iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara kuimarisha mikakati ya kibiashara kwa wafanyabiashara wa Zanzibar , wakubwa wakati na hata wadogo wadogo ili kuweza kuwainua kibiashara.
Alisema Wizara ya biashara na viwanda itachukua juhudi za kushirikiana katika mipango ya kuzalisha bidhaa zilizobora na zenye kiwango jambo ambalo litatasaidia kuwaongeza nguvu ya kuyatumia masoko ya afrika mashariki.
Aidha aliitaka jumuiya hiyo kuyatumia masoko ya afrika mashariki ikiwemo kongo sudan msumbiji kenya ili kukuza kiwango cha kibiashara hadi ikifika julai mwakani iwe tayari matunda yameshaonekana.
Hata hivyo alimpongeza Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chamber of commerce) Toufiq S.Turky kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Afrika Mashariki.
Nae Rais wa Jumuiya ya (chamber of commerce) Toufiq S.Turky alisema gharama zinazotozwa zaidi ya mara tatu kwa mizigo zinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya kibiashara.
Alifahamisha kuwa iwapo matatizo ya usafirishaji wa bidhaa utapofanyiwa marekebisho kwa utasaidia kukuza kiwango cha kibiashara ambacho kitafikia ushindani wa kibiashara katika afrrika ya mashariki.
Saturday, October 19, 2019
Home
/
Top News
/
Chamber of commerce watakiwa kuingia katika ushindani wa kibiashara Afrika Mashariki
Chamber of commerce watakiwa kuingia katika ushindani wa kibiashara Afrika Mashariki
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment