Adbox

Sunday, October 20, 2019

Viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika Lindi waanza ''kuzitapika'' fedha walizokwapua

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika mkoani Lindi wameanza kurejesha fedha za wakulima wa ufuta ambazo wanatuhumiwa kuzichukua na kusababisha wakulima hao kushindwa kulipwa.

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbugo, jana alipozungumza na waandishi wa habari katika manispaa ya Lindi.

Brigedia Jenerali Mbugo alisema jumla ya shilingi 255,598,194.00 kati ya shilingi 1,207,832,091.00 zinazotakiwa kurejeshwa, tayari zimerejeshwa.

Alisema baada ya kurejeshwa kiasi hicho, bado shilingi 964, 728,397.00 hazijareshwa. Kwahiyo mkurugenzi huyo amewataka viongozi wa vyama ambao bado hawajetekeleza agizo la mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli la kuwataka warejeshe, watekeleze agizo hilo haraka.

Brigedia Jenerali Mbungo alisema taarifa iliyotelewa na naibu waziri wa kilimo, mheshimiwa Hussein Bashe  na kukabidhiwa TAKUKURU ilionesha  wakulima wa zao hilo wamedhulumiwana vyama kumi vya msingi vya ushirika jumla ya shilingi 436,869,982.00. Hatahivyo baada ya kufanyika ufuatiliaji, taasisi hiyo imebaini kwamba kwa mkoa wa Lindi pekee vyama 31 vya msingi vya ushirika(AMCOS)  vimewadhulumu wakulima wa zao hilo jumla ya shilingi  1,236,364,075.00.

 '' Wa-Tanzania  wanapaswa wafahamu kuwa kwa kipindi cha siku 3 kuanzia Oktoba 16,2019 hadi Oktoba, 19, 2019 TAKUKURU imefanikiwa kurejesha shilingi 255,598,194.00 ambazo ni sehemu ya fedha walizodhulumiwa wakulima wa ufuta na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika 31,'' alisema Mbungo.

Katika hali inayodhihirisha TAKUKURU haitanii katika utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Rais, kaimu mkurugenzi mkuu wake huyo alisema '' Ili kuthibitisha kuwa TAKUKURU haina utani, inaendelea na zoezi la kutambua, kupiga picha na kukamata mali za viongozi wa AMCOS. Ambazo zinazodaiwa kama amana ya madaeni wanayodaiwa, na endapo viongozi hao watashindwa kukamilisha malipo ya fedha wanazodaiwa kwa wakati uliowekwa na walivyohaidi kwa maandishi,basi mali hizo zitataifishwa kwa mujibu wa sheria ili wakulima walipwe fedha zao,'' alisisiti Brigedia Jenerali Mbungo.

Alionya kwamba hakuna chama kinachodaiwa ambacho kitabaki salama. Kwani zoezi la ufuatiliaji huo ni endelevu.¥ Aliweka wazi miongoni mwa sababu za kufanyika zoezi hilo ni dhuluma waliyofanyiwa kutovumilika kutokana na ukubwa wake. Kwahiyo serikali ya awamu ya tano kupitia vyombo vyake. Ikiwemo TAKUKURU  haitasinzia wala kulala hadi itakapo hakikisha na kujiridhisha kwamba fedha zote walizodhulumiwa wakulima hao zimerudishwa na kulipwa kwa wenye haki nazo( wakulima).

No comments:

Post a Comment

Adbox