Adbox

Friday, October 18, 2019

Vigogo kampuni ya katani matatani

Viongozi watano wa Kampuni ya Katani Limited ya Tanga akiwemo mkurugenzi wa zamani wa kampuni hiyo, Salum Shamte wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kushindwa kulipa madai ya wakulima wadogo wa Mkonge kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 29 kwa kipindi cha miaka 19.

Viongozi hao ni pamoja na mkurugenzi wa sasa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mkurugenzi wa zamani wa kampuni hiyo aliyejulikana kwa jina la Juma Shamte.

Uamuzi huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi maalum wa kampuni hiyo ya Katani kuhusu madai ya wakulima.

No comments:

Post a Comment

Adbox