. Timothy Itembe, Mara
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imesema kuwa haitozi kodi mara mbili wafanyabiashara badala yake wanaotoza kodi hiyo mara mbilimbili ni halmashauri za wilaya kwa lengo la kukuza mapato ya halmashauri.
Afisa Elimu na huduma ya mlipa kodi mwandamizi mkoani Mara, Zake Wilbard Rwiza alisema hayo jana kwenye kikao cha semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa ajili ya kutoa elimu juu ya kodi ya ushuru mbalimbali 2019-2020 iliyofanyikia ukumbi wa Moroni Gardeni.
Rwiza alisema hayo baada ya wafanyabiashara kuhoji ni kwasababu gani wanatozwa kodi marambilimbili katika biadhaa mbalimbali wanazokuwa wamezinunua huku wakizisafirisha ndani ya wialaya na mkoa kwa lengo la kuuza.
Rwiza alifafanua kuwa kuna haja wafanyabiashara kupeleka malalamiko hayo mbele ya wawakilishi wao ambao ni madiwani wanaowachagua ili kuwawakilisha na kuwatetea.
Mmoja wa wafanyabiashara hao ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa viwanda na kilimo TCCIA,Steven Chacha Kisengewa alisema kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara waliowengi kutokuwa na elimu ya mlipa kodi na kutofautisha kodi za serikali kuu na kodi zinazokusanywa na serikali za mitaa kwaajili ya maendeleo ya halmashauri.
Kisengewa alitumia nafasi hiyo kuishauri Mamlaka ya mapato kuongeza kasi ya kutoa elimu kwanjia ya semina ya mikusanyoko lengo likiwa ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya huduma kwa mlipa kodi pamoja tunajenga Nchi.
Naye Bhoke Nyamohanga mfanyabiashara wa duka la bidhaa mbalimbali alibainisha kuwa wanatozwa ushuru marambilimbili njiani wanapokuwa wameenda kununua bidhaa Mwanza hali ambayo inaleta kero.
Friday, October 11, 2019
TRA wajivua lawana kutoza kodi mara mbili
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment