Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji "Mo Dewji' ameikumbuka siku ambayo alitekwa na watu wasiojulikana.
Mo kupitia mtandao wa Instagram, ameandika ujumbe ambao anakumbuka siku tisa ambazo alitekwa huku akiwa amefungwa macho na mikono.
"Mwaka mmoja uliopita siku kama ya leo nilitekwa. Siku 9 nilizofungwa macho na mikono kilikuwa ni kitendo cha mateso zaidi kwenye maisha yangu yote. Kutokuwa na uhakika wa kuona dakika inayofata nikiwa hai ilikua ni hali ya kutisha, lakini nashukuru Mwenyezi Mungu, na sala za wengi, nilivuka shida zote," ameandika Mo.
"Kurudi kwangu salama ndio ushuhuda wa kweli wa nguvu ya maombi! Nilibarikiwa kwa kupewa nafasi ya pili ya maisha. Asanteni Watanzania wenzangu wote na kila mtu duniani kote kwa maombi yenu na msaada usio na shaka. Mwenyezi Mtukufu awasimamie katika mambo yenu kwa upendeleo mkubwa! Ameen," ameongeza.
Friday, October 11, 2019
Mo Dewji akumbuka mwaka mmoja wa kutekwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment