Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amewatahadharisha wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma kuwa makini na vitendo vya utapeli vilivyoibuka vya kutumia jina la Mkuu huyo wa TAKUKURU kutapeli watu.
Akizungumza na Muungwana Blog ofisini kwake, Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuna vitendo vya utapeli vimeibuka, watu hao wakiwatumia viongozi mbalimbali ujumbe wa simu na au kuwapigia simu wakidai wao ni wakuu wa TAKUKURU, na katika Ofisi zao Kuna Mambo hayako sawa hivyo watoe fedha, kuweka sawa Mambo hayo.
" Wananchi na viongozi wawe makini Sana Kuna watu wanatuma sms wakidai ni wakuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, na katika Ofisi yake kuna Mambo hayako sawa, hivyo watoe fedha kurekebisha Mambo hayo yawe sawa" amesema.
Amesema tangu mwezi wa tatu mwaka huu mpaka sasa amepokea malalamiko manne kutoka maeneo mbalimbali wakidai kuwa wamepigiwa simu na Mkuu wa TAKUKURU kuwa watoe fedha ili kurekebisha Mambo yao katika Ofisi hizo.
Hivyo amewataka wananchi na viongozi wawe makini na vitendo hivyo, TAKUKURU inafanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria katika kutekeleza majukumu yao na kama Kuna tatizo mtu anahojiwa ofisini na sio kupigiwa simu, na malipo ya kisheria yanalipwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha amesema TAKUKURU mkoani wa Dodoma imepokea malalamiko nane(8) toka kwa wananchi wa Kata mbalimbali za wilaya za Mkoa wa Dodoma zenye viashiria vya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.
Amebainisha kuwa taarifa hizo zimewasilishwa na wakazi wa maeneo tofauti,baada ya kubaini baadhi ya wagombea watarajiwa wakishinikiza majina yao yapitishwe kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
"Mpaka sasa nimepokea malalamiko nane yenye viashiria vya rushwa nasi tunayafanyia kazi kujiridhisha kama malalamiko hayo yanaukweli sheria itachukua nafasi yake," amesema Kibwengo.
Amesema kutokana na elimu wanayoendelea kutoa umekuwa na manufaa, kwanza wananchi wa maeneo mbalimbali kutoa taarifa, amesema kuna taarifa nyingine zina toka vijiji vya ndani kabisa lakini Takukuru ikifuatilia inabaini kweli malalamiko hayo yana mashiko.
Thursday, October 31, 2019
TAKUKURU Dodoma yatoa tahadhari utapeli kumuhusisha mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment