Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo kwa Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba, zinawasilisha taarifa zote zinazohusu mashauri ya madai zinazohusiana na taasisi hizo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, ameyasema hayo leo jumatano, wakati akifungua mkutano baina yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za
Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Zaidi wa wajumbe 300 kutoka taasisi hizo wamehudhuria Mkutano huu ambao ni wa siku mbili, unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma,akiwamo pia Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt.Clement Mashimba (SG).
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,taarifa hizo zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Profesa Kilangi, amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba, Ofisi yake imeamua kutoa maelekezo hayo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi
zake bila taarifa ya uwepo wa kesi hizo kuwasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Changa moto hii ya baadhi ya Taasisi kuendesha kesi zake pasipo kutoa taarifa kwa Ofisi hizo mbili kumeisababishia serikali hasara ambayo ingeweza kuzuilika.
“Ipo changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi zake bila taarifa kuwasilishwa Ofisi ya yangu na ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ,utaratibu huu umeisababishia hasara serikali hasara ambayo inegeweza kuzuilika”.
“Hivyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo kwa taasisi zote za serikali kuwasilisha taarifa zote za mashauri ya madai kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Mkuu wa Serikali kwa hatua zake stahiki.Amesisitiza AG.
Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Ofisi yake pia ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa mfumo maalum wa kieletroniki wa uwasilishaji wa taarifa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka katika Taasisi mbalimbali baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara na Taasisi zake.
Vile vile Profesa Kilangi ameeleza kwamba, Ofisi yake imesajili Jarida litakalochapisha masuala Muhimu ya sheria yanayohusu Mihimili ya Dola ( The Journal of Government Law). Lengo la
jarida hilo litakuwa ni kutoa fursa kwa mawakili wa Serikali kuchapisha makala mbalimbali zinazohusu mihimili ya Dola.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Kilangi ameitisha Mkutano huu kwa madhumuni kadhaa yakiwamo ya kuiwezesha Ofisi yake kujadiliana na kubadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Taasisi hizo juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na uoaji wa huduma za kisheria hapa nchini.
“Kama mnavyofahamu jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kutoa ushauri katika masuala yote ya kisheria jukumu ambalo pia nyinyi mnalifanya kwa katika maeneo yenu kwa niaba ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivyo kikao hiki ni muhimu sana kwetu sote ili tupeane taarifa na miongozo mbalimbali inayohusiana na utekelezaji wa majukumu hayo kwa lego la kuongeza tija na ufanisi wa kazi". Akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kuhusu kuanzishwa kwa Daftari la Mawakili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Kifungu cha 16A kama
ilivyorekebishwa, inampa mamlaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzisha Daftari la Mawakili wote walioko kaitka Utumishi wa Umma nchini ( Rolle of State Attorneys).
Akasema, Daftari hilo, litakuwa lina taarifa mbalimbali za Mawakilil hao na pia litasaidia sana kufahamu wakili gani yupo wapi na ana taaluma gani au amebobea katika fani gani ili hatimaye pale serikali inapomhitaji kwa jambo fulani aweze kupatikana kwa urahisi.
Aidha kupitia Dafteri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataweza kutambua mahitaji ya aina ya mafunzo kwa ajili ya kuongeza uwezo na ubobezi wa mawakili wa Serikali katika maeneo mbalimbali.
Mada mbalimbali zikiwalishwa katika siku hii ya kwanza ya mkutano zikiwamo zinazohudu vazi maalum ( joho) litakalovaliwa na Wanasheria wa Serikali wanapokwenda Mahakamani au katika
shughuli maalum za kitaaluma.
Lengo la kuwa na Joho maaluma kwa Mawakili wa Serikali wanaokwenda Mahakamani pia litawezesha kutambuliwa kirahisi kwa Mawakili wa Serikali, pia litawaongezea kujiamini, kuaminika na kukubalika.
Thursday, October 31, 2019
Taasisi za serikali zatakiwa kuwasilisha taarifa za kesi za madai
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment