Adbox

Wednesday, October 30, 2019

Serikali kuendelea kuwekeza katika mawasiliano

Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kuwekeza katika mawasiliano kama mkakati mmojawapo wa kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda inafikiwa

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo amesema sekta ya mawasiliano ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.

"Kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 sekta ya mawasiliano ilikua kwa asilimia 13.1 na ilikuwa sehemu ya pili katika kuchangia ukuaji wa uchumi nchini," amesema Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako amesema katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika mpaka vijijini, mwaka 2014 serikali iliingia mkataba na kampuni kutoka Vietnam wa kuhakikisha huduma hiyo inafika katika vijiji 4,000 ambapo kufikia Januari 2019, vijiji vyote vilikuwa vimefikiwa na huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox