Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi na James Buchard Rugemalira, wamemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuomba msamaha na kukiri mashitaka ya uhujumu uchumi ikiwemo la kutakatisha Sh.Bil 309.
Mapema jana taarifa ya kwanza kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa inayomuhusu Seth ambapo ilielezwa ameandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu wa Gereza baada ya msamaha uliotangazwa na Rais Magufuli.
Kuhusu Rugemarila, Wakili wa utetezi, Michael Ngaro anayemtetea Rugemalira amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kuwa mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi yanayomkabili na kwamba mpaka sasa hawajapata majibu na akauomba upande wa mashitaka kufanya mchakato ili wapate majibu ya barua hiyo haraka
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa, ni kweli wamepokea barua za washtakiwa wote wawili na kwamba zinafanyiwa kazi na watapatiwa majibu, Hakimu Shaidi ameah
Friday, October 11, 2019
Rugemalira aungana na Sethi, aandika barua kwa DPP kuomba msamaha
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment