Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Damian Mgaya mwenye umri wa miaka 41 anadaiwa kutoroka Hospitalini hapo kufuatia tuhuma za kumbaka mgonjwa ambaye ni Binti wa miaka 16, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo amethibitisha tuhuma hizo na kusema kesi imefikishwa katika kituo cha polisi.
Mama Mzazi wa Msichana huyo anasema siku ya tukio Muuguzi alifika katika wodi namba 3 na alipoona mgonjwa hali yake si nzuri aliomba aondoke nae akambadilishie dawa, walipofika ofisini kwake alimchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku hadi saa nane usiku na kisha kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi akiwa hajitambui na amemwagiwa maji mwili mzima.
"Ni kweli tukio lipo na sio mara ya kwanza siku za nyuma Mgaya akiwa kituo cha afya cha Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hii ni mara ya pili na huu ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kanuni za kiutumishi"- Dkt.Ruta Deus, Mganga Mkuu wa Wilaya
Friday, October 18, 2019
Muuguzi wa Hospitali anadaiwa kumbaka mgonjwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment