Adbox

Friday, October 18, 2019

Mkuu wa majeshi ya ulinzi CDF, General Venance Mabeyo ameongoza kamati ya ulinzi na usalama Taifa kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji

Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wametembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuhakikisha mpaka huo na wananchi wa maeneo hayo wako salama, hatua hiyo imekuja baada ya kusemekana nchini Msumbiji kunavitendo vinavyoashilia Ugaidi vinaendelea nchini humo hayo yamesemwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini CDF, General Venance Salvatory Mabeyo, huku akisisitiza kuwa kwa sasa mpaka uko salama na wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kuendelea na majukum yao ya kila siku.

Aidha kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema hali ya nchi kwa sasa ni salama na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuendelea kudumisha amani na usalama nchini.

No comments:

Post a Comment

Adbox