Adbox

Saturday, October 26, 2019

Mamia ya abiria wakwama Korogwe

Mamia ya Wananchi (abiria) waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani na waliotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali wamekwama tangu jana mchana wilayani Korogwe na Handeni Mkoa wa Tanga sababu zikielezwa ni kutokana na maji kupita juu ya daraja la Mandera na kulisomba daraja la Handeni mkoani humo.

Wakizungumza na leo,  Jane Mathias na Juma Kombo wamesema tangu jana saa 5 asubuhi wamekwama katika daraja hilo kutokana na wingi wa maji uliotokana na mvua inayoendelea kunyesha mkoani Tanga.

"Tumefika hapa jana saa 5 asubuhi hadi muda huu (leo saa1 asubuhi) hatuoni uwezekano wa kuvuka," amesema Mathias.

Kombo ameiomba Serikali kuondoa adha hiyo kwa sababu kwa wiki mbili sasa daraja la Mandera limekuwa likijaa maji.

"Ni aibu barabara muhimu kama hii watu kukwama kutokana na daraja kujaa maji, kila siku wanajenga vivuko hawaimarishi  barabara," amesema Mathias.

No comments:

Post a Comment

Adbox