Adbox

Sunday, October 27, 2019

Korea Kaskazini yadai hakuna mafanikio kwenye mahusiano yake na Marekani

Korea Kaskazini imesema leo hakuna mafanikio yaliyopatikana kwenye mahusiano yake na Marekani na kwamba uadui ambao ungeweza kuyatumbukiza mataifa hayo vitani bado unaendelea.

Hayo ni kwa mujibu wa Afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, Kim Yong Chol, ambaye amenukuliwa akisema Marekani imekuwa ikiishinikiza Korea Kaskazini kwa njia za kibabe badala ya kuzingatia wito wa Pyongyang wa kulegeza msimamo wake.

Yong Chol aliyekuwa mjumbe wa Korea Kaskazini katika mazungumzo ya nyuklia, amesema itakuwa ni kosa kwa Marekani kupuuza kipindi cha mwaka mmoja kilichotolewa na kiongozi wa Korea Kaskazini ili kuimarisha mahusano kati ya mataifa hayo mamwili.

Kim Jong Un ametenga tamati ya mwaka 2019 kuwa muda wa mwisho kwa mazungumzo na Marekani juu ya kuukongoa mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Adbox