Adbox

Friday, October 18, 2019

Jenerali Mabeyo avishukuru vyombo vya Habari

Na. Ahmad Mmow, Nanyumbu

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi( CDF), Jenerali Venance Mabeyo amevishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari kwamuwezesha kuiona shule ya msingi ya Michiga B iliyovyokuwa na hali mbaya ya miundombinu.


Jenerali Mabeyo ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya ufunguzi na kukabidhi vyumba sita vya madarasa, vyumba vya vitatu vya ofisi za walimu na matundu 26 ya choo katika shule ya msingi Jenerali Venance Mabeyo ambayo awali ilikuwa inaitwa Michiga B.

Hafla hiyo ilifanyika katika kijiji cha Pachani, kata ya Michiga, wilaya ya Nanyumbu, mkoa wa Mtwara.

Kamanda Mabeyo alisema bila ya vyombo vya habari kuibua changamoto zilizokuwepo katika shule hiyo ambayo sasa ni mlezi wake asingejua chochote kuhusu shule hiyo ambayo imepewa jina lake kutokana na mchango mkubwa aliotoa katika ujenzi wa shule hiyo.

"Niliona kupitia vyombo vya habari, sikuamini kama ni shule. Maana iliezekwa kwa nyasi, madawati yake ni chanja. Ndipo nilipoguswa na kuona nisaidie walau chumba kimoja cha darasa katika kusaidia kutatua changamoto hizo," alisema Jenarali Mabeyo.

Aidha aliwataka walimu wa shule hiyo wahakikishe inafanya vizuri kulinda heshima ya jina lake ambalo limepewa shule hiyo. Akiweka wazi kwamba atahakikisha anafanya mambo yakipekee mbayo yataonesha utofauti.

"Tofauti ya kwanza ni ushirikiano baina walimu na wananchi. Lakini kubwa zaidi kiwango cha ufaulu, kwahiyo walimu fanyeni juhudi ili wanafunzi wafaulu. Haitapendeza shule hii iwe na jina langu halafu iwe ya mwisho," alisema Mabeyo.

Amehaidi kushirikiana na wananchi kutatua changamoto zitakazo jitokeza kwenye shule hiyo. Huku akiwaasa watunze na kulinda miundombinu ya shule hiyo kwa kuwa na mpango endelevu wa matumizi ya vyumba hivyo.

Ujenzi wa shule hiyo ambao umefikia 98% ukikadiriwa kutumia takribani shilingi 68 milioni unafanywa na vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wa Kambi ya Jeshi namba 843( 843 KJ) iliyopo katika wilaya ya Nachingwea. Ambapo vifaa vya ujenzi kwakiasi kikubwa vilitolewa na Jenerali Mabeyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox