Adbox

Tuesday, October 29, 2019

Anayedaiwa kumteka Mo Dewji, aomba kufutiwa shtaka

Wakili wa utetezi, Mahfudhu Mbagwa, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kufuta shtaka la kutakatisha  fedha linalomkabili dereva taksi, Mousa Twaleb (46), ili mshtakiwa huyo aweze kupata dhamana.

Twaleb ambaye ni mkazi wa Tegeta na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kumteka nyara mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji katika kesi ya uhujumu uchumi namba 42/2019.

Mbagwa amewasilisha ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, wakati kesi hiyo ilipowasilishwa kwa ajili ya kutajwa.

Amewasilisha ombi hilo baada ya wakili wa Serikali, Daisy Makakala kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na jalada halisi la kesi hiyo lipo Polisi.

Makakala baada ya kueleza hayo, wakili Mbagwa alisema anaomba shtaka la kutakatisha fedha liondolewe katika hati ya mashtaka ili mteja wake apate dhamana.

“Kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umechukua muda mrefu kukamilika, naomba upande wa mashtaka mfute shtaka la kutakatisha fedha ili mteja wangu aweze kupata dhamana,” ameomba Mbagwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox