Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene amemuagiza Katibu Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuta vibali vyote vya zamani vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu.
Simbachawene amesema kuundwe tume ambayo itasimamia utengenezaji wa vibali vipya vitakavyokidhi matakwa ya kibiashara.
Ametoa agizo hilo, jijini Dar es salaam wakati akiongea na wafanyabiashara wa Vyuma chakavu ambapo amesema vibali vyote vilivyotolewa awali vimefutwa na utaratibu wa kuboresha vibali hivyo utafanyika upya ndani ya siku Saba.
“Kamati iundwe ndani ya masaa 24 na iweze kufanya kazi kwa siku saba kukamilisha hivyo vibali vipya, Nemc muwasikilize wafanyabiashara na kuzingatia ukusanyaji wa tozo ili kukuza uchumi wa nchi.”amesema.
Thursday, September 5, 2019
Waziri Simbachawene aagiza vibali vya zamani kufutwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment