Adbox

Friday, September 6, 2019

Suala la maiti kuzuiliwa Hospitalini kutokana na madeni lajadiliwa Bungeni

Utaratibu wa kulipia gharama za matibabu kabla ya ndugu kuchukua maiti leo umehojiwa na wabunge katika kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma.

Swali kuhusu jambo hilo lilianza kuulizwa na mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Susan Lyimo. “Lini Serikali itaacha kutoza gharama miili ya wanaofia hospitali na kuhifadhiwa ili kupunguza simanzi kwa wafiwa,” amesema Lyimo.

Akijibu swali hiyo, naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndungulile amesema miili ya wanaofia hospitali husika au kuletwa kutoka maeneo mbalimbali inatakiwa kuwekwa kwenye majokofu yenye ubaridi na wakati mwingine kuwekwa dawa za kusaidia isiharibike.

“Panapotokea changamoto au mwananchi kushindwa kumudu gharama za afya ikiwa ni pamoja na matibabu na hata huduma za uhifadhi wa maiti, mwananchi huyu anapaswa kutoa taarifa kwenye uongozi wa hospitali husika ili kupata maelekezo ya namna ya kutatua changamoto hiyo,” amesema.

Ili kuondokana na changamoto hizo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewahimiza wananchi kujiunga na Bima ya Afya kwa lengo la kupunguza gharama za matibabu toka mfukoni

No comments:

Post a Comment

Adbox