Na.Thabit Madai, Zanzibar.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika ambao unaofanyika Zanzibar katika Hoteli ya Madinat Al Bahri utakuwa wa kwanza kuwashirikisha wajumbe wengi zaidi wa kanda hiyo.
Mkutano huo unahudhuriwa na Maspika,Manaibu Spika na Wabunge zaidi ya 400 kutoka Mabunge ya Nchi mbali mbali za Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Madinat Al Bahri, Spika Ndugai alisema takwimu zinaonyesha idadi kubwa ya wajumbe wanaoshiriki mikutano hiyo ni 250 lakini mkutano wa Zanzibar utawashirikisha zaidi ya wajumbe 350 ambao ni sawa na asilimia 90 ya wajumbe wote wa Kanda hiyo.
Alisema wajumbe wa mkutano huo kutoka mataifa wanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika walianza kuwasili toka tarehe 30 na tayari vikao vya Kamati mbali mbali vimekuwa vikiendelea.
Aliongeza kuwa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika itakutana leo Jumapili kukamilisha taratibu za mkutano huo .
Alisema kuwepo kwa idadi kubwa ya wajumbe katika Mkutano huo inatokana na sifa kubwa iliyonayo Zanzibar ya usalama na amani, ukarimu kwa wageni na vivutio vya Utalii.
Aliwataka wananchi na wafanyabiashara wa Zanzibar kuitumia fursa ya kuwepo kwa mkutano huo kutoa huduma bora wanapohitaji huduma katika maeneo yao na kuendelea kutangaza vivutio vipya vya utalii viliopo Zanzibar.
Spika wa Bunge alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein atafungua rasmi mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kesho Jumatatu katika Hoteli hiyo.
Mkutano huo huwa unafanyika kila mwaka katika nchi mbali mbali, Mkutano huo kwa mwaka huu umekuja na kauli mbiu isemayo ”Bunge Mtandao kwa ajili ya kuwawezesha Democrasia”
Sunday, September 1, 2019
Home
/
Top News
/
Spika Ndugai - Mkutano wa 50 wa chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola umevunja rekodi
Spika Ndugai - Mkutano wa 50 wa chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola umevunja rekodi
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment