Adbox

Thursday, September 5, 2019

Serikali yawasilisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Bungeni

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Serikali imewasilisha Muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali(Na.4) wa mwaka 2019(The wrriten laws Miscellaneous Amendments (No.4) act, 2019) ambayo inapendekeza kufanya marekebisho kumi na moja (11).

Akisoma Muswada huo mbele ya Bunge, Jijini  Dodoma,   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi, amesema muswada huo unalenga kwenda kufanyiwa marekebisho sheria takribani kumi na moja.

Amezitaja baadhi ya sheria ambazo vinalengwa kwenda kufanyiwa marekebisho kuwa ni , “sheria ya mawakili, sura 341, sheria ya vizazi na vifo, sura ya  108, sheria ya mwenendo ya mashauri ya jinai,  sura ya 20, sheria ya urejeshwaji wa wahalifu, sura ya 368” .

“Sheria ya mashauri dhidi ya serikali, sura ya 5, sheria ya mahakama za mahakimu, sura ya 11, shera ya taifa ya mashtaka, sura 430, sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, sura 329, sheria ya mapato  yatokanayo na uhalifu, sura 256, sheria ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, sura 268, na sheria ya chama cha msalaba mwekundu, Tanganyika, sura ya 66”, amesema Profesa, Kilangi.

No comments:

Post a Comment

Adbox