Adbox

Thursday, September 5, 2019

Kituo maarufu cha redio nchini Zambia chasitisha kupiga muziki wa Afrika Kusini

Nchini Zambia , kituo maarufu cha redio kimesema kuwa hakitapiga tena muziki wa Afrika kusini kupinga mapigano ya ubaguzi ambayo yanaendelea Afrika Kusini .

"Hot FM imesitisha kupiga muziki aina yoyote ulioimbwa na msanii wa Afrika Kusini," Kituo hicho kimeandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Facebook.

"Mataifa yote ya Afrika yalisimama mstari wa mbele kuisaidia Afrika Kusini walipokuwa na shida," redio hiyo ilisema ikinukuu Umoja wa Afrika.

Wakati wa mapigano dhidi ya ubaguzi wa rangi , makao ya chama tawala cha Afrika Kusini(ANC) yalikuwa Zambia .

"Afrika ni moja ingawa sasa wenzetu Afrika Kusini ndio wameamua kuleta ubaguzi tena,

Tunapinga uvamizi wa chuki za kibaguzi dhidi ya ndugu zetu unaoendelea katika katika nchi hiyo ."

Siku ya Jumatano , maduka kadhaa katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka yalifungwa wakati wanafunzi walipoingia barabarani kuandamana kupinga vurugu zinazoendelea Afrika Kusini,

Chama cha mpira wa miguu kilisitisha mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini ambayo ilitarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi mjini Lusaka.

No comments:

Post a Comment

Adbox