Adbox

Tuesday, September 3, 2019

RC Makonda awasilisha mapendekezo ya muswada wa mabadiliko ya sheria ya mirathi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Septemba 3 ametimiza ndoto za wajane kwa kukabidhi Muswada wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Mirathi kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwaajili ya Kufanyiwa maboresho na kufikishwa Bungeni.

Akikabidhi muswada huo mapema leo, Jumanne jijini Dodoma, Makonda amesema ndani ya muswada huo ameainisha mapendekezo ya kubadilishwa kwa sheria kandamizi ambazo zimekuwa mwiba na mateso kwa wajane kwa miaka mingi.

Aidha Makonda amesema miongoni mwa Sheria kandamizi anazopendekeza zifanyiwe mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya Mirathi ya Mwaka 1865, Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini ya Mwaka 1963 kwa kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa na mapungufu mengi ya kisheria.

No comments:

Post a Comment

Adbox