Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Magufuli amemkuta Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi akiwa anaendelea vizuri tofauti na hali ilivyokuwa alipomtembelea tarehe 10 Septemba, 2019 siku aliyoletwa MOI akitokea Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro alikougua ghafla baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.
Akiwa MOI, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi amefanyiwa upasuaji na timu ya Madaktari Bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa mafanikio na sasa anaendelea vizuri.
Mhe. Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na kuimarika kwa hali ya Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi na amewapongeza Madaktari Bingwa wa MOI kwa kumtibu kwa mafanikio makubwa.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi, Baba Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Padre Dkt. Alister Makubi wamesali sala ya pamoja ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wapone haraka.
Baada ya kutoka MOI, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akiwemo Baba Mzazi wa Daktari wa Rais, Mzee Wilson Ngwale aliyelazwa hospitalini hapo.
Tuesday, September 24, 2019
Rais Magufuli amjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment