Adbox

Wednesday, September 25, 2019

Polisi wakemewa kuwahukumu watuhumiwa hadharani 'unatafuta sifa?'

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amekemea, kuonya na kutoa mwongozo kwa Maofisa wa chombo hicho wafuate dira yake kwa kuwa anayeweza kushika cheo alichonacho ni “mtu mmoja tu” na muda wake ukifika ataondoka.

Hotuba hiyo ya Kamanda Sirro pia iligusia maofisa ambao wamekuwa wakiwahukumu watuhumiwa katika mikutano na waandishi wa habari.

“Huwa nashangaa. Wakati mwingine hivi unamchukua mtuhumiwa, unamuweka pale unamuonyesha kila wakati. Unatafuta sifa?” alihoji.

“Hivi kwenye upelelezi katika mazingira ya kawaida huyo si mtuhumiwa tu? Leo unamtoa hadharani kaiba, unasahau kesho na keshokutwa. Kwenu huko Musoma anakushtaki kwamba kuna siku ulinidhalilisha mimi kuwa mwizi. Vitu vingine tushauriane, si ndiyo.”

No comments:

Post a Comment

Adbox