Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amewapigia chapuo wanawake kupewa nafasi ya kugombea ubunge wa kuchaguliwa badala ya viti maalumu ambavyo amesema vinawafanya kuonekana kama daraja la pili.
Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Tamasha hilo linalenga kuwaleta pamoja wahanarakati wa haki za binadamu kutafakari na kusherehekea mafanikio, kubadilishana mawazo na uzoefu, kubaini changamoto.
Jaji Warioba alisema kuwa anafikiri sasa umefika wakati taifa liamue kwa dhati kwamba katika utekelezaji wa mambo kutakuwa na 50 kwa 50 na kwamba ili kufikia hilo inabidi kuiangalia sheria ya uchaguzi ili iweke utaratibu ambao utahakikisha kwenye uchaguzi uwiano huo unafikiwa.
“Itafika mahali sasa hatutakwenda uwakilishi wa uwiano ili uwe na uhakika kwamba tangu uteuzi utapata 50/50, hilo tuanze kulifikiria maana tutakuwa tunazungumza hivi viti maalumu vinamfanya mbunge kama ‘second class’ (daraja la pili).
“Nadhani mpaka sasa hivi sheria yetu inasema kuwa Waziri Mkuu lazima uwe umechaguliwa. Kwa hiyo hawa wenye viti maalumu hawana sifa za kuwa Waziri Mkuu, kwanini? Mimi nadhani sasa kama taifa tuzungumze tuamue tuwe na utaratibu ambao utawahakikishia 50/50,” alisema Jaji Warioba.
Alisema nguvu ya Watanzania iko kwenye umoja, mshikamano na uzalendo na taifa lina amani.
Wednesday, September 25, 2019
Jaji Warioba atoa neno kw a Wanawake kuhusu kugombea Ubunge
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment