Na Thabit Madai, Zanzibar
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amesema amepokea kwa moyo mkunjufu mabadiliko ya uteuzi yaliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kwamba uamuzi huo haujakosewa.
Ayoub amesema kuwa uwamuzi uliofanywa na Rais na Serikali haujakosewa na upo sahihi kwa mujibu wa katiba na Sheria na yeye ameupokea kwa Moyo Mkunjufu.
Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 23 katika hafla maalumu ya makabidhiano ya Ofisi na Mkuu wa Mkoa wa Mpya wa Mjini Magharib Unguja Hassan Khatibu Hassani ambapo hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Vuga.
Ayoub ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja alisema kuwa uteuzi huo aliofanywa na Rais ni heshima kubwa waliyopewa kwao hivyo ni wajibu wao kuendelea kuwatumikia wananchi haijalishi wapi alipopangiwa kazi.
“Nimepokea kwa moyo Mkunjufu kabisa uteuzi huu na tayari tumeshaapishwa kilichobaki kuwaomba wafanyakazi ninao waacha katika mkoa huu kutoa mashirikiano ya hali na mali kwa Mkuu huyo Mpya wa Mkoa”Alisema Mkuu wa Mkoa wa Kusin Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud.
Aliongea kusema kuwa wafanyakazi na watendaji wa Serikali na chama ndani ya Mkoa huo hawana budi kutoa ushirikiano na Mkuu huyo wa Mkoa ili kuongeza kasi ya ukuaji wa Maendeleo ndani ya Mkoa huo.
“Nafahamu kuwa mabadiliko yoyote huja na Chanagamoto zake ila Rai yangu kwenu kubadilisha changamoto hizo kuwa fursa za kimaendeleo, naamini kuwa mutampa mashirikiano kama niliyoyapa mimi ” alisema Ayoub.
Katika maelezo yake Ayoub alimueleza Mkuu wa Mkoa Mpya wa Mjini Magharib Unguja kuwa katika uwongozi wake ndani ya mkoa huo walianzisha mambo ambayo hayamo katika sheria ni kutokana na mahitaji ya mkoa.
“Mambo hayo sisi tuliyaanzisha kutokana na mahitaji ya mkoa katika kuwahudumia wananchi, hivyo ukiyapenda unaweza kuyaendeleza na kama hautayapenda basi utayaacha si lazima uyaendeleze” alieleza Ayoub.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa Mpya wa Mjini Magharib, Hassan Khatib Hassan alisema kuwa ataendeleza yale yote mazuri aliyoyakuta ndani ya mkoa huo atayaendeleza ili kuchochea Maendeleo.
“Nakuahidi kuyafanya yale ambayo yote uliambia na kuhusu jambo la uhalifu linalofanywa na baadhi ya vijana ndani ya mkoa huu nitaanza nao kuwashughulikia” alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjiini Magharib Unguja Hassan Khatib Hassani.
Aliongeza kusema kwa kuomba mashirkiano na watendaji wa ofisi hiyo ili kuendeleza yale yote mazuri ambayo yaliachwa na Mkuu wa aliyepita.
Hafla hiyo ya Makabidhiano ya Ofisi yalihudhuriwa na kamati ya ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya ndani ya Mkoa huo na wafanyakazi ofisi hiyo ya mkoa wa Mjini.


No comments:
Post a Comment