Na Timothy Itembe Mara
Msimamizi wa Uchaguzi halmashauri ya Tarime Vijijini,Peter Nyanja amesema kuwa kama ikitokea matukio ya majanga ya asili kama vile kunyesha Mvua ni sababu moja wapo ya kuhairisha uchaguzi kwa muda hadi itakapokoma kunyesha.
Nyanja alisema hayo jana katika kikao cha pamoja kilicho washirikisha Wadau mbalimbali wa uchaguzi serikali za mitaa 2019 wa kutoka Vyama vya siasa,wakuu wa madhehebu ya Dini wazee maarufu pamoja na wazee wa mila.
Kwa mjibu wa kifungu cha 201A cha sheria za serikali za mitaa (Mamlaka za wilaya)sura ya 287zikisomwa pamoja na kanuni ya 9(1) na (2) ya kanuni za mwenyekiti wa kijiji na wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji za mwaka 2019 zilizotolewa kwa tangazo la serikali namba 373 ya tarehe 26,04,2019.
"Kampeni za uchaguzi zitaanza saa mbili kamili asubuhi na zitamalizika saa kumi na mbili kamili jioni yakila siku ya kampeni vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la polisi Mgambo mwenye sare au Afisa anaye simamia ulinzi vitatumika katika kihakikisha kunakuwepo na hali ya usalama na ulinzi katika mikutano ya kampeni na wakati wa uchaguzi kwa ujumla na vituo vya kuandikisha wapiga kura vipo 500," alisema Nyanja.
Mmoja wa wadau kutoka kanisa laWasabato,Samsoni Gesase alikumbusha wajumbe wa kikao hicho kuwa kuna kuwepo mara nyingi mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuzingatia matukio ya majanga ya asili kama vile Mvua na mengine ambayo yanaweza kutokea wakati na siku ya kupiga kura ili zichukuliwa tahadhari ambapo msimamizi wa uchaguzi kwa nafasi aliyopewa anatakiwa kulichukulia tahadhari jambo hilo ili yanapotokea hayo kuwepo na majibu mbadala.
Gesase alitumia nafasi hiyo kupongeza uongozi awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuwa maandalizi mazuri ya uchaguzi 2019 ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa Uhuru na haki ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaonya wale wote ambao wanatabia ya kuvuruga uchaguzi kuwa waache tabia hiyo mara moja.
Naye Mwenyekiti wa Chadema wilaya Tarime,Mwita Joseph alisema kuwa sheria,Taratibu na kanuni ikiwemo Katiba ya Jamuhuri ya muungano ya Tanzania vyote kwa pamoja havina kamosa makosa yanatokea kwa wasimamizi kutozingatia yaliyomo.
Joseph pia alitumia nafasi hiyo kupongeza mchakato mzaima pamoja na maandalkizi ya uchaguzi kuendelea kutolewa semina kwa walengwa ili kujua haki zao zakupiga kura lakini Joseph akawa na wasiwasi juu ya mkuu wa wilaya kuhusika moja kwa moja katika uchaguzi hali kanuni na sheria za uchaguzi hazijamtaja mkuu wa wilaya ni mhusika.
Tuesday, September 24, 2019
Mvua kunyesha chanzo cha kuhairisha kupiga kura kwa muda
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment