Adbox

Sunday, September 29, 2019

Mpishi akamatwa na polisi kwa tuhuma za kutumia bangi kama kiungo cha kuongeza ladha

Mpishi mmoja nchini Italia amekamatwa kwa tuhuma za ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya polisi kugundua bangi nyumbani kwake.
Vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti kuwa, mpishi ambaye anashiriki katika kipindi cha runinga anayefahamika kwa jina la Carmelo Chiaramonte, alipatikana na mimea miwili mikubwa ya bangi na kilo moja ya Indian hemp.
Kwa mujibu wa polisi wa nchini humo wamedai kuwa mvinyo uliochanganywa na bangi, zaituni, kahawa, na samaki aina ya tuna pia vilikusanywa nyumbani kwake karibu na Catania huko Sicily Mashariki.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, limesema kuwa mpishi huyo aliwaeleza maafisa wa polisi kwamba alikuwa anajaribu viungo vipya vya upishi.
Chiaramonte amesema yeye ni mshauri wa vyakula asili kwa upishi wa kileo
Hata hivyo mpishi huyo mwenye miaka 50, anayeishi katika kijiji cha Trecastagni, chini ya Mlima Etna ameachiwa huru huku kesi ikisubiriwa kuwasilishwa mahakamani.
Chiaramonte ni mpishi katika hoteli ya Katane Palace huko Catania, hupika vyakula vya watu wa Meditarenia kwa mujibu wa maelezo kwenye mtandao wake.
Alishiriki kipindi cha mapishi kwenye televisheni kuhusu “historia ya mazao na utamaduni wa kilimo cha Sicily”, La Sicilia limeripoti.
Mojawapo ya vipindi vyake kiliitwa ‘Upishi uliokosa nidhamu’ na ‘vyakula vya kutia hamu ya tendo la ndoa’, gazeti hilo limesema.

No comments:

Post a Comment

Adbox