Adbox

Monday, September 2, 2019

Mafunzo ya Ujasiriamali kuzinduliwa Bagamoyo na Katibu Mkuu UVCCM

Vijana zaidi ya 500 wilayani Bagamoyo wanatarajiwa Kunufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Kambi maalum itakayofanyika mwezi Septemba Katika Kijiji cha mandera Wilayani Bagamoyo.

Kambi hiyo iliyopewa jina  la "Kambi Moto" inatarajiwa kufanyika kwa siku 10 na itaanza rasmi Septemba 3, mwaka huu na kufunguliwa na Katibu wa UVCCM Taifa, Mwl Raymond Mwangala ambapo pamoja na Mafunzo ya ujasiriamali, vijana hao watashiriki Shughuli mbalimbali  za  kijamii ikiwemo  ujenzi wa Darasa pamoja na Kuanza Ujenzi wa ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo.

Mwenyekiti wa  Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi Uvccm, Mkwayu Makota, amewataka Vijana kuchangamkia Fursa hiyo kwakua mafunzo hayo yatawaongezea maarifa mengi yatakayowasadia Kujiajiri.

"Tunawashukuru sana Viongozi wetu wa ngazi zote Za Vijiji,Madiwani ,Wabunge na Wakurugenzi  pamoja na mkuu a Wilaya kwa namba wanavyotupa Kipaumbele Vijana hasa kwenye Kupigania Mikopo ya Vijana nasi kama Umoja wa Vijana tumeona ni vyema Tuanzishe Kambi hii  ili kuzidi kuongezeana maarifa " alisema  Mkwayu Makota

No comments:

Post a Comment

Adbox