Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Kazi ya Mtendaji wa Kata ni kubwa, watu wasiidharau.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Watendaji wa Kata kutaka katika Mamlaka ya Serikali za kata zote Tanzania Bara katika Bustani za Ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.
"Kazi ya Mtendaji wa Kata ni kazi kubwa, msiidharau, kuna walioanzia kwenye nafasi hiyo na wakapanda mfano tulikuwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Joseph Kakunda, alikuwa ni Mtendaji wa Kata ya Manzese, kidogo kidogo mtapanda," amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa “Nyinyi ni wasimamizi wa Watumishi wa Umma kwenye Kata, hata kama kwenye Kata yako kuna Waziri,Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya usiogope kumwandikia mapendekezo kama anaenda kinyume na maadili ya kazi zake,na ukimuona mkubwa sana nitumie nakala na mimi."
Monday, September 2, 2019
Kazi ya Mtendaji wa Kata ni kubwa, msiidharau - Rais Magufuli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment