Kipa Juma Kaseja amesema kuwa haoni nafasi ya timu ya Taifa ya Sudan kuibuka na ushindi dhidi ya Taifa Stars leo usiku katika Uwanja wa Taifa.
Stars watavaana na Sudan katika mchezo muhimu wa kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), ambapo mchezo wa kwanza utapigwa leo hii jijini Dar na mchezo wa marudiano utapigwa nchini Uganda kati ya Oktoba 18.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kaseja alisema, wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo na Sudan kwa kuwa mara ya mwisho wanacheza na Sudan walishinda kwa mabao 2-1 hivyo anadhani hata awamu hii wanakwenda kupata ushindi na kutengeneza njia nzuri ya kufuzu.
“Tutawafunga Sudan katika mchezo huu tutakaocheza nyumbani, tumekuwa na matokeo mazuri kwa mwaka huu tukiwa katika Uwanja wa Taifa, pia hata mchezo wa mwisho tulivyocheza nao, tuliwafunga kwa mabao 2-1, hivyo nafikiri watanzania waendelee kutusapoti nina uhakika mwaka huu tutafuzu,” alisema Kaseja ambaye ni mchezaji pekee wa Stars aliyepo kikosi kwa sasa ambaye amecheza Simba na Yanga.
Sunday, September 22, 2019
Kaseja afunguka kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Sudan
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment