Adbox

Saturday, September 28, 2019

Balozi Mahiga atoa neno kuhusu Utawala bora

Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania,  Balozi Augustine Mahiga  amesema Serikali inayojisifia kuzingatia utawala bora lazima itoe fursa ya wananchi  kupata taarifa sahihi huku akisema kuwa taarifa hizo ni zile zinazomuwezesha raia kuchukua uamuzi bora na sahihi.

Ametoa kauli hiyo leo Mkoani Morogoro katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya upataji taarifa ambayo kitaifa yameandaliwa na mtandao wa vyombo vya habari vya jamii Tanzania (Tadio) kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco).

Balozi Mahiga amesema upatikanaji na utoaji wa taarifa ni sehemu ya utawala bora unaojumuisha masuala mbalimbali ikiwemo demokrasia, kutaka taarifa kutumika vyema kwa manufaa ya wananchi.

"Unaweza kuchukua uamuzi mbaya kama huna taarifa ya kutosha katika jambo fulani, hivyo tukisema kupata taarifa ni pamoja na kutoa mchango katika kutengeneza Serikali bora," amesema.

Amebainisha kuwa taarifa ni sawa na panga lenye makali pande zote mbili, upande mmoja linaleta haki na mwingine kuleta uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment

Adbox