Waziri wa Madini, Dotto Biteko amezitaka kampuni zinazofanya utafiti wa madini zizingatie sheria ili kuepuka utoroshaji wa madini nchini.
Waziri Biteko ametoa agizo hilo katika kijiji cha Nditi, wilaya Nachingwea, mkoa wa Lindi alipotembelea mgodi uliopo katika kijiji hicho.
Biteko aliyetoa agizo hilo baada ya kuona madini yaliyotajwa kama sampuli iliyopatikana kutokana na utafiti unaofanywa na kampuni ya Ngwena, alisema kwa mujibu wa marekebisho ya sheria yaliyofanywa mwaka 2017 ni marufuku kampuni kutunza au kusafirisha sampuli bila kibali kilichotolewa idara ya utafiti( GST) ya wizara ya madini.
Alisema kitendo cha kusafirisha sampuli za madini bila kupata kibali cha GTS licha kuwa nikosa, lakini pia kinaweza kusababisha mashaka kutoka kwa wananchi ambao wataamini kuwa sampuli hizo nimadini yanayotoroshwa na kampuni hizo. Hali ambayo inawezakusababisha tafrani pindi wananchi wakizuia yasafirishwe.
"Mkiitwa hamtokei, leseni zenu zikivamiwa mnakuja na maelezo mengi, vizungu vingi. Ila kwenye vitu hivi hamfanyi na hamuwi wazi,'' alisema Biteko.
Mbali na hayo, waziri huyo mwenye dhamana ya madini amezitaka kampuni za madini kuweka wazi ushirikiano wake na kampuni za nje. Ambapo baada ya kuweka wazi zinatakiwa kusajiliwa wizarani.
Biteko ambaye pia alitoa agizo hilo baada ya kugundua kampuni ya Ngwena inashirikiana na kampuni ya nje inayotambulika kwa jina la Indiana bila kufuata sheria na taratibu. Kwani kampuni hiyo haionekani popote kwenye nyaraka zilizopo kisheria.
Alisema serikali haikatai kampuni za nje, lakini zifuate sheria. Kwani inapotoa leseni kwa kampuni za kizalendo inaamini ni mali ya wazawa. Hata hivyo baadhi yake zinazibeba kampuni za nje kinyume cha sheria.Kitendo ambacho kinasababisha serikali kukosa na kupoteza mapato.
''Exchange( Makabidhiano) ya mkono yanasababisha serikali kutopata chochote, mnamalizana wenyewe lakini kunafedha zinatolewa na kampuni hizo, serikali haipati chochote. Indiana tutamuona wapi, leseni inaonesha ni kampuni ya Ngwena,'' alihoji Biteko.
Kutokana na hayo aliyoyaona katika mgodi wa Nditi, amezitaka kampuni zinazoshirikiana na kampuni za nje ambazo hazijasajiliwa wizarani ziende zikasajiliwe haraka kwa mujibu wa sheria. Kwani kuna ukweli usio na chembe ya shaka kwamba baadhi zinatumia fedha za kampuni za hizo Kwahiyo zinatumiwa na kampuni hizo kinyume cha sheria.
Tuesday, August 13, 2019
Waziri Biteko ashtukia janja ya makampuni ya Madini
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment