Adbox

Tuesday, August 13, 2019

Uwanja wa ndege wa Hong Kong wafunguliwa tena

Uwanja wa ndege wa Hong Kong umefunguliwa tena baada ya kusitisha safari zote za ndege hapo jana kutokana na maandamano. Mamlaka ya uwanja huo hata hivyo imeonya kwamba baadhi ya safari zitaendelea kuathirika, baada ya China kusema kuwa shughuli za waandamanaji uwanjani hapo zilionyesha dalili za ugaidi. Tangazo hilo limewekwa kwenye huduma ya simu ya mkononi, au app ya uwanja huo mnamo saa kumi na mbili asubuhi saa ya Hong Kong. Ingawa viongozi wa uwanja huo wamewalaumu waandamanaji kwa kufungwa kwa safari, sababu halisi ya hatua hiyo haiko bayana, kwa sababu waandamanaji hao hao wamekuwa wakiikalia sehemu ya kuwasili kwa wasafiri kwa hali ya utulivu kwa muda wa siku tano zilizopita. Wengi wa waandamanaji wameondoka usiku wa leo, wakibaki wapatao 50 tu. Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa wasafiri wapatao 100 walikuwa wamepiga msitari kwenye ofisi ya shirika la ndege la Cathay Pacific asubuhi ya leo.

No comments:

Post a Comment

Adbox