Adbox

Saturday, August 10, 2019

Watu mashuhuri Tanzania watoa pole kufuatia ajali ya Lori la mafuta



Baada ya watu kuungua moto na kupoteza maisha baada ya gari la mafuta kulipuka na kuwaka moto Msamvu Itigi mkoani Morogoro. Watu mashuhuri Tanzania watoa pole kufuatia ajali hiyo;

"Tumepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu ajali ya lori la mafuta,  Morogoro, iliyosababisha moto na kuunguza watu kadhaa. Mkuu wa Mkoa na timu za uokoaji wanaendelea kukabiliana na  hali katika eneo la tukio. Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae," Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.

"Nimepokea kwa Mshtuko  Mkubwa ajali mbaya ya MOTO iliyotokea Msamvu Morogoro na kusababisha VIFO na MAJERUHI wengi!! Pole sana kwa ndugu, jamaa na marafiki.  Pole sana kwa Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa MSIBA HUU MKUBWA. Mungu awapumzishe kwa AMANI!😭😭!," ameandika Halima Mdee.

"Nina toa  pole kwa msiba mkubwa uliotokea huko Morogoro kwa ajali na kulipuka kwa gari la mafuta na kusababisha vifo/vilema.Natoa wito kwa Mamlaka za Serikali kuchukua hatua kwa Polisi/Fire Morogoro,kwa uzembe mkubwa ktk kusimamia ajali ya aina hii haswa baada ya kuwa imetokea," Lema.

"Poleni Sana Ndugu Zetu Wa Morogoro kwa msiba huu mzito. Mungu Azilaze Roho Za Marehemu Wote Mahali Pema Peponi. Amen," ameandika Jokate Mwegelo.

"Poleni saa Ndugu zangu wa MOROGORO...Mwenyez Mungu azipe nguvu Familia zote katika kipindi hiki kigumu kwao, awaponye haraka majeruhi wote na kuzilaza roho za Marehem mahala pema peponi Amin," Diamond Platnumz.

"Mungu azilaze roho za ndugu zetu mahali pema peponi," ameandika Shilole.

"Nawaombea waliotangulia mbele za haki pumziko la milele na majeruhi wapone haraka," ameandika Bdozen.

"Tuwaombee na Majeruhi wote wa ajali hii kubwa wapone haraka," ameandika Haji Manara

No comments:

Post a Comment

Adbox