Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amesema mwanawe wa kiume ambaye pia ni mbunge Eduardo Bolsonaro pamoja na waziri wa mambo ya nje wako nchini Marekani kujadili uwezekano wa Marekani kutuma msaada Brazil kufuatia moto unaosababisha uharibifu katika eneo la msitu wa Amazon.
Bolsonaro ameeleza kwamba amemuomba rais Donald Trump kuisaidia nchi yake lakini rais huyo wa Marekani alimfahamisha kuwa hawezi kuchukua uamuzi bila ya kupata ombi la Brazil.
Kiongozi wa Brazil amesema mwanawe wa Kiume Eduardo na waziri wa mambo ya nje Ernesto Araujo wako kwenye mazungumzo na rais Trump.
Bolsonaro anafikiria kumteua mwanawe huyo wa kiume kuwa balozi nchini Marekani ingawa nafasi hiyo itahitaji kuidhinishwa na bunge la Brazil.
Friday, August 30, 2019
Rais wa Brazil amtuma mwanawe na waziri wa nje kuzungumza na Trump
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment