Na.Rahel Nyabali, Tabora.
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora imemuhukumu Fabian Francis Mkazi wa Kaliua, kutumikia kifungo cha miaka ishirini na miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za Serikali ndani ya hifadhi ya msitu wa Ugalla wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Awali katika mwenendo wa shauri hilo Wakili upande wa Jamhuri Tito Mwakalinga aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa Fabian Francis alikamatwa ndani ya hifadhi ya ugalla wilayani Kaliua eneo la Upango mnamo tarehe 2 January 2019 akiwa na nyama ya wanyama wa Porini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne na silaha ndogo kinyume cha Sheria ya hifadhi ya wanyamapori namba tano ya mwaka 2009.
Akisoma hukumu katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba sita la mwaka 2019 Hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Tabora Chiganga Mashauri Tengwa amedai kuwa maamuzi hayo ya mahakama yamefikiwa baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili na kujiridhisha pasipo shaka yoyote kwamba mshitakiwa Fabian Francis amehusika kutenda makosa mawili baada ya kukutwa ndani ya hifadhi ya msitu wa Ugalla akiwa na nyara za Serikali nyama ya wanyamapori.
Friday, August 30, 2019
Ahukumiwa miaka ishirini Jela
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment